Jumapili 26 Aprili 2026 - 23:00
Kata’ib Sayyid al-Shuhada watoa onyo kwa Marekani na Israel: Muqawama hautakaa kimya mbele ya uchokozi

Hawza/ Ofisi ya kitamaduni ya Harakati ya Muqawama ya Kiislamu ya Kata’ib Sayyid al-Shuhada ndani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kutoa taarifa rasmi kujibu kuwekwa kwa zawadi kwa ajili ya kumuua katibu mkuu wa kundi hilo, ilitangaza: Hatua dhidi ya Hajj Abu Alaa al-Wala’i ni shambulio dhidi ya mhimili wa muqawama, na vitendo kama hivyo vitakabiliwa na majibu makali.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, matini ya taarifa ya ofisi ya kitamaduni ya Kata’ib Sayyid al-Shuhada ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kama ifuatavyo:

Bismillahi ar-Rahmani ar-Rahim

﴿وَیَمْکُرُونَ وَیَمْکُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَیْرُ الْمَاکِرِین.﴾

Sisi katika Muqawama wa Kiislamu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhada tunaamini kwamba; hatua yoyote ya kudhalilisha au kushambulia mmoja wa makamanda wakuu ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na vitisho dhidi ya eneo hili na kushinda makundi ya kigaidi, ni ukiukwaji wa wazi wa mamlaka ya Iraq na haki za watu wake. Mwenendo na hatua za hivi karibuni za Marekani dhidi ya Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhada, “Hajj Abu Alaa al-Wala’i”, ni vitendo ambavyo kwa mtazamo wetu vinachukuliwa kuwa ni shambulio dhidi ya mkusanyiko mzima wa muqawama.

Kwa njia hii tunazionya nguvu za Marekani na utawala wa Israel kwamba; hatua hii na ukosefu huu wa heshima hautabaki bila majibu, na athari zake zitazikumba kambi na maslahi ya Marekani katika eneo hili. Sisi kama wafuasi wa Mtume wa Uislamu (saww) na Ahlul-Bayt (as), hatuoni kifo isipokuwa kuwa ni heshima, na tunatangaza kwa maadui kwamba vitisho vya kifo havitatuogopesha.

Ofisi ya kitamaduni ya Kata’ib Sayyid al-Shuhada ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Inafaa kutajwa kwamba serikali ya Marekani imetangaza kuweka zawadi ya dola milioni 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kutambuliwa au kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la “Kata’ib Sayyid al-Shuhada” la Iraq.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha